Tuesday, May 22, 2007

Aisha Mbaga

MbagaMambo vupi mpenzi msomaji wa safu hii ya mahaba? natumai kwa uwezo wa Mungu amekujaalia pumzi na umzima wa afya hapo ulipo unaungana nami katika mambo ya mahaba.
kama ilivyo ada ya mapenzi kuwa ni makubaliano kati ya wawili basihakuna haja ya kulazimishana katika kufanya mapenzi, hii ndiyo mada yetu ya leo.
Ukipendana na mtu kwa dhati, mtaheshimiana, hutafanya kitu chochote cha kumwuudhi au kumwuumiza, hutamlazimisha mwenzio kufanya kitu ambacho hapendi au hataki na wakati wote utataka kumfurahisha.
Kitu kimojawapo ambacho kitakutokea wakati unakua ni kuwa na mpenzi aliyekuingia moyoni au kupata mapenzi mazito.
Kumpenda mtu kunaweza kuwa kuzuri. Lakini mara nyingine kunaweza kukuchanganya akili hususan yanapojitokeza mambo ya kufanya mapenzi.
Wapo ambao wanafurahia mapenzi kwa kuwa wanapendana na wenzi wao lakini pia wapo wanaotamani kufa ama kujuta kuzaliwa kwa kuwana wapenzi ambao hawajatulia.
Ili kuepukana na majonzi hakikisha kuwa unayempenda naye anakupenda kisha hana papara ya ngono.
lama kwli anakupenda atakuvumilia nawe hakikisha kuwa unakuwa na msimamo wa kutofanya ngono hadi uwe tayari. ZIngatia mambo yafuatayo ikimpata mpenzi ili kuhakikisha kuwa unamsoma na kuupa moyo wako nafasi ya kufanya maamuzi.
LAZIMA MFANYE NGONOUkiwa na mpenzi unayempenda kwa dhati haina maana kwamba ni lazima mfanye nae mapenzi. Kitendo cha kufanya mapenzi kinatakiwa kiheshimiwe na kipewe hadhi yake kwa hivyo usikiendee kwa papara!
SUBIRI mpaka ukiwa tayari kimaumbile na kimawazo. Unaweza kuanza kufanya mapenzi ukiwa katika mapenzi ya dhati na ambayo unayaona yanaweza kumudu vishindo vyote.
USIKUBALI KUDANGANYWAUkiangalia filamu karibu zote zinazooneshwa siku hizi au ukizungumza na marafiki zako unafikiria kwamba kila mtu anafanya mapenzi wakati wote. Hii sio kweli kabisa! Watu wengi wanasubiri mpaka watakapokuwa watu wazima au wakishaolewa au kuoa.
EPUKA UONGO KATIKA MAPENZIUwapo utaweza kuwa mkweli kwa huyo unayemtarajia, ni wazi kuwa mnaweza kuelewana na ni rahisi sana kugundua tabua zake kwa kuwa wakati wote utakuwa mwazi kwake naye atajutahidu kuwa wazi na ukiona mpenzi wako ni mwongo basi hakufai tafuta njia ya kumfanya awe mkweli ama heri kukaa na kumtafuta mkweli kwani baadae unaweza kujutia mahusiano yako.
Unaweza kumpenda mpenzi wako na kuamua kutofanya naye mapenzi. Kama mpenzi wako anakupenda kwa dhati basi ataheshimu uamuzi wako na atakuwa mkweli kwako ikiwa ni pamoja na kukutunzia heshma yako.
pamoja na mila na desturi za Waafrika, mwanamke ameonekana kwa yeye ndiye anayelazimishwa kufanya ngono wakati hawako tayari, Hata wavulana wanalazimishwa kufanya mapenzi na wapenzi wao au hata marafiki zao. Sio vizuri kwa marafiki kuwashawishi wasichana au wavulana kufanya mapenzi wakati wao hawako tayari.
basi kwa leo tuoshie hapa ila usisahau kujiunga nami wiki ijayo,kwa waswaki na maoni wasiliana namoi kwa barua pepe yangu aishamudysaan@yahoo.com.
Na Aisha Mbaga
Mambo vipi msomaji wangu wa safu ya Mahaba? Natumai kwa uwezo wa Mwenyezii Mungu umzima wa afya na waendelea vyema katika maandalizi ya mwanzo wa wiki.
natumai wiki iliyopita tuliangalia jinsi ya maandalizi ya wakati wa tendo la kujamiaana.
ninaimani nimeeleweka kwa wale waelewa. nawashukuru walionipigia simu kunipongeza na kunitaka ushauri.
Dada yangu salha wa Arusha ananiuliza jinsi ya kumlea Mwanaume, usijali, Salha kwani mwanaume mbele ya mwanamke ni sawa na mtoto mdopgo, waweza mliza upendavyo ila unachotakiwa ni kuwa mbunifu.
Leo tutazingumzia mambo muhimu katika kufikisha hisia zako. wapo baadhi ya watu hawawezi kumweleza mwanaume ukweli kuwa anampenda na matokeo anabaki akiumia bila kujua la kufanya. kwa upende wangu mimi sioni aibu endapo najikuta nipo penzini nakiwa mwazi.
jambo la kufanya kwa mwanaume umpendaye naye hajui kuwa unampenda, kwanza mwambie kama uwezo wa kufanya hivyo unao. wapo wanawake jasiri kwa kuweka mambo bayana na kujikuta wengine wanafanikiwa kutatua matatizo yao. baadhi ya watu wanaamini kuwa, kumweleza mwanaume ukweli kuwa unampenda ni utamaduni wa wazungu, mimi naamini kuwa katika hisia hakuna mzungu wala mwafrika.
Endpo huwezi kuweka mambo bayana tumia nwiki wako kuhakikisha kuwa unamteka mwanaume huyo kwa kumtega kwa kutumia njia tano muhimu
njia ya kwanza kuweza kumtega mwanaume ni mavazi.
unaweza kumtega mwanaume unayempenda kw akuimia mavazi, jaribu kuvaa vivazi vya kumvutia na kumfanya atahamaki kwa kukuwaza kila amapo kumbuka kivazi chako.
fanua jitikada za kujipitisha pitisha kila mara kwake huku ukiwa na vizawadi ambavyo vitamfanya awe rafuki yako na kumweleza wazi kuwa unapenda kuwa karibu naye hatakama hataki kuwa mpenzi wako.
jia ya pili, pendelea kutoka naye kila wakati ikiwa ni moja ya njia ya kumhamasisha na utokapo kuwa unamshangaza kwa kumpa zawadi ama kumwandalia chakila maakum ambacho unauhakika atakipenda na kitamvutia.
tumia sauti yako katika mazungumzo ili aweze kuvutika nayo kwani katika mahusiano, sauti inaweza kuchukua nafasi kumshawishi mwanaume na kujikuta akiiwaza na kuingia mtegoni.
pia hakikisha kuwa macho yako yanazungumza kwa kumtazama na kila ayaonapo ataona vimrlea vya mapenzi ndani ya mboni ya jicho lako na kujikuta kuwa anasogea karibu na wakati mwingine anaweza kukushangaza kwa kukuambia kuwa anakupenda japo hakuwa tayari kuwa na wewe.
wakati mwingine si lazima mwanaume aanza kupenda hata wanawake wanapenda na wananafasi ya kuonyesha mapenzi yao na kuhangaika hadi kufanikisha penzi lake kw ayule ampendae.
kwa leo tuishie hapo na usikose kuungana nami wiki ijayo. Alamsiki
kwa maoni na ushauri wasiliana nami kwa simu 0755690690, ama barua pepe yangu aishamudysaan@yahoo.com pia unaweza kupitia website yangu, mudysaa.blogspot.com

Sunday, May 13, 2007"UKIWEZA FANYA UNACHOKITAKA" Usikubali kurudishwa nyuma.
Nawatakia watoto wenzngu wote maisha mema. na wale waishio katika mazingira magumu, mungu awasaidie waweze kuodokana na maisha hayo. nawaasa wamuombe mungu atawasaidia. wafadhili na matajiri wajitokeze kuwalea watoto hao ili wasijiingize katika makundi yasiyofaa.

Mtoto Kaysaan, anapenda kumsalimu kaka yake na kumweleza kuwa, anampenda sana na anamtakia afya njema na masomo mema. pia Kaysaan anamsalimia bibi yake Neema Saidi Mkenga na Familia nzima ya Mzee aidi Mkenga wa Usangi Mwanga. Hakuishia Hapo anamsalimu Mamayake Mpendwa Aisha Sarumbo na kumtakia maisha mema yenye furaha wakati wote, Ujumbe anapenda kumwambia mama yeke kwa awalee kwa mapenzi waweze kupata elimu na upendo kwa wengine. anaedelea kumsalimu baba yake na kumwasa kuwa , Dunia ni Tambara bovu yampasa kuwa makini na maisha yake.
TUPENANE MIMI NA KAKA YANDU AHMEDYSAAN TUWEZE KUPATA BARAKA ZA MUNGU>

Friday, May 11, 2007

Na Aisha Mbaga Je sunna ni ndevu, masharubu, nguo, kilemba, au muonekano wa mavazi?
Hivi nini yawezekana kuwa ndiyo Sunna ya Rasulullah?
Sunna ya Allah yani SUNNATILLAH ni nini?
Wenye ufahamu mdogo wanajua sunna kuwa ni operesheni wanayofanyiwa watoto wa kiume.
Ufahamu wa sunna wa wenye ufahamu wa wastani ni mpana kidogo... Kwao, sunna ni Ndevu, masharubu na mavazi!... Kwao, kumfuata Rasulu wa Allah ni kujitumbukiza katika mavazi ya miaka 1400 iliyopita; kufuata mila na desturi za kipindi hicho!..
Hawa ni waislam wenye kusema kwamba wao ndiyo waislamu na wale wenye kuvaa mashati ya mikono mifupi si waislamu!
Hawa ni kama waislamu waliomuua Kiongozi wa Uwalii, Mlango wa elimu Hazrat Ali!... Ufahamu wao, ni ufahamu uliomuona huyu swahaba mkubwa ametoka nje ya dini!.
Tafitini yaliyosemwa na Hazrat Muhammad alayhissalaam kuhusu Hazrat Ali... Muelewe hali na kiwango cha ufahamu wa waislamu ambao walimuona yu nje ya njia ya Rasulullah!
Watofautisheni ambao, kwa madai ya kuhudumia dini na sunna wamefanya dini ufalme na wamekuwa wakiitumia DINI kutawala watu.
Nimeamua nilifafanue jambo hili wazi wazi baada ya kuona habari kwenye ukurasa wa internet ulionukuu ufafanuzi nilioufanya!
Nawaomba mfikirie vizuri nitakayoyaeleza...
Nilipokuwa na miaka 20 yani miaka 40 iliyopita, nilimuota Rasulullah akaniambia niende kwa Hazrat Abubakar... Kilichofuata si muhimu hapa... Na mimi baadae mwaka huo nikaandika maisha ya Hazrat Abubakar... Baadae nikaandika kidogo maisha ya Hazrat Rasulallah ya kipindi cha Makka kwa kuambatanisha na hadithi katika kitabu nilichokiita “Muhammed Mustafa” alayhissalam.
Nimeandika haya kwa sababu ifuatayo. Nilitafiti kwa undani sana maisha ya wakati huo... Nilisoma karibu Hadithi 60 sahihi.
Kama inavyojulikana Rasul wa Allah Muhammed Mustafa alayhissalaam alizaliwa ndani ya kabila la Kureishi lililokuwa na upapatikiaji wa Masanamu... Babu, na ndugu zake wengine walikuwa wenye kufuata taratibu za kabila...
Rasulullah akakulia humo... ALIVAA kama wao, ALIACHA NDEVU kama wao, ALIFUNGA KILEMBA kama wao!. Alikaa, kusimama, kula na kunywa kama wao...
Aliendelea hivyo mpaka alipofikisha miaka 39 akawa Rasulu wa Allah!... Kama Rasulu wa Allah alibaini ukweli katika umri huu; Ulipokamilika UNABII miaka mitatu baadae, akaanza kuwafahamisha watu yakufanya kwa mujibu wa Wahyi aliopata, ili wajichumie kwa ajili ya maisha yao ya milele.
HAKUBADILI NDEVU WALA MAVAZI YAKE katika kipindi hiki wala baada yake!
Aliendelea kufunga kilemba kama wao, alivaa kama wao, na kuzunguuka na ndevu kama wao!. Hata ile nguo yake yenye rangi nyingi na bakora yake aliendelea nayo!..
Sunna ya Rasulu wa ALLAH ni sunna ya makusudio ya jina “ALLAH” ambaye ndiye Rasulu wake; “SUNNATILLAH”!.
Hata sisi tukiielewa “SUNNATILLAH” na kuifuata tutakuwa tumeifuata sunna ya Rasulullah na tutakuwa kwenye “SUNNATILLAH”! Lakini si kwa ndevu, masharubu, nguo na vilemba!
VILEVILE JAMBO MUHIMU LINALOBIDI LIBAINIKE NI:
Rasulullah hakuingilia wala kuwashauri kuhusu mavazi na desturi wapapatikia masanamu wakina Abu Jahil, Abu Lahab na mfuwasi wao ambaye alimuua mjukuu wa Rasulullah, Yazid; Aliendelea kuwa ni mwenye kuvaa kama wao. Kwa sababu hili halikuwa na umuhimu katika kufanikisha yanayotakikana na DINI; na wala halina uhusiano na ukweli wa maisha ya milele au kujulikana kwa makusudio ya jina “ALLAH”
Na hii inamaanisha kwamba...
ALLAH akimuongoza mtu, mtu huyu anaweza akaendelee kuvaa kwa mujibu wa mila na desturi za jamii yake, lakini hatofuata jamii yake katika mambo yanayohusika na “SUNNATILLAH”; Na ataendelea kuufahamisha ukweli aliojifunza unaohusika na uongofu alioupata!.
Hii inamaanisha, si kupinga mila na desturi katika mambo kama mavazi, bali kuendelea nayo ndiyo SUNNATIRASUL!.
Kwa sababu DINI haikuja kwa ajili ya mapinduzi ya muonekano wa mavazi ya watu! Si kazi ya Dini kushughulika na muonekano wa mavazi. Kwa mujibu wa suna, watu wana haki ya kuvaa, kusoma, kuishi, na kufanya kazi kufuatano na imani zao bila kuharibu amani ya jamii! Hata kama hili litakuwa liko kinyume kwa wale ambayo mbongo zao hazijaelewa!
Kutoa hukumu juu ya dini ya mtu kwa kuangalia mavazi yake ni ishara tosha ya mtu asiyeendelea mwenye ubongo wenye kufuata mkumbo.
Rasulu wa kusidio la jina “ALLAH”, kwa kuwafahamisha watu ukweli wa utaratibu na mfumo wanaoishi ndani yake, alijitahidi kuwafanya waishi kwa mujibu wa mfumo na utaratibu wa ALLAH ambao ulipewa jina la “DINI”, na hivyo basi kuwa wenye kujiandaa na maisha ya milele!
“MTU WA DINI” ni yule aliyetafiti, kuuliza na kuuelewa utaratibu na mfumo wa ALLAH na kukubali kuishi kwa mujibu wake!. MTU WA DINI kutokana na mfumo huu aliouSOMA anakuwa “MUTTAQI” yani mwenye kuchukua tahadhari dhidi ya hatari zinazokuja alizozibaini!.
Kufuata sunna ya Rasulu wa Allah maana yake ni kuuthamini ufahamu wake, kudumu katika njia aliyoionyesha na kwa kufanya aliyosema kufikia mambo mazuri yanayokuja. Maana yake ni kuuvumbua uhakika wa kiini chake; na kufanikisha matokea yake ya kusisimua!. Sio kufuja maisha kwa kufuata mkumbo.
Kufuata sunna ya Rasulu wa Allah maana yake ni kuchanga na watu bila malipo elimu aliyozawadiwa. Siyo kuwaliwaza watu na riwaya za muonekano wa mavazi!.
Mtu aliyeuelewa mfumo na utaratibu wa Allah yani “SUNNATILLAH” na kisha akafanywa yanayopaswa anakuwa ndiyo mtu aliyefuata “SUNNATIRASULULLAH”!.
Onyo la kwamba “Atakayejifananisha na kundi lolote basi atakuwa miongoni mwao” linamaanisha kwamba mtu yupo katika jumuia ambayo anachangia nayo Fikira na Imani... na si ufanano wa mavazi au ndevu!.
Kama tulivyo eleza katika makala yetu yenye kichwa “Kutawala watu kwa kutumia dini”, kuna baadhi ya watu wamepiga marufuku udadisi na utafiti wa DINI; na hivyo basi wamepelekea ukuaji wa watu wenye mbongo kama kaseti, wenye kuiga na wasio na uwezo wa kufikiri.
Dunia ni pahala pa hekima na kila ufafanuzi wa Rasulullah umelala kwenye hekima fulani!. Mtu mwenye akili ni yule mwenye kuuliza na kutafiti kila jambo ili kumuelewa vizuri Rasulullah na kujaribu kuifikia hekima ya lililofundishwa.
Hili limeashiriwa na onyo la kwamba “hekima ni kitu kilichopotezwa na mumin”
Yeyote aliye na mgongano wa mawazo au mapengo katika mfumo wake wa kufikiria, ni mfuata mkumbo ambaye hajailewa dini na hajaweza kuuSOMA ufanyajikazi wa utaratibu na mfumo aishio ndani yake.!.
Ukweli ni kwamba DINI haikubali ufuataji mkumbo!.
Kuiga matendo kunazaa matokeo yanayofanana; lakini hili haliwezekani kwa kuiga mawazo !.
Kuwa “Faqih” yani mwenye ueleo, ni Lutufu(upendeleo) ya Allah. Hivyo mtu anaacha kuwa mwenye kufuata mkumbo. Hata siku moja kukumbuka kanuni za FIQIH hakumaanishi kuwa “FAQIH”.
Uwezo wa kuhifadhi vitu kichwani umepoteza thamani baada ya uvumbuzi wa kaseti!.
Dini imefahamishwa kwetu kuwa ni yenye kustahili kusomwa ili ubaini utaratibu na mfumo unaoishi ndani yake; la muhimu zaidi “UJIFAHAMU MWENYEWE” ! Uivumbue hazina iliyo katika uhakika wako; Na mwisho ufahamu kusudio la jina ALLAH kwa mujibu wa elimu ya holografia na kuijua nafasi yako katika ulimwengu.. Wale ambao hawajalielewa hili katika maisha yao hawajaisoma “IHLAS” Hata kama wameirudia mara laki!...
Tulifikirie vizuri onyo la Rasulullah kwamba, “Kuna mwenye kuswali sana lakini hajaambulia lolote isipokuwa uchovu; kuna mwenye kufunga sana lakini zaidi ya njaa hajapata faida yoyote”
Rasulu wa Allah ametufahamisha Quran ili tuielewe na kutafakari. Tufanye hivyo hadi ufike wakati ambao hatua zote tunazochukua maishani ziwe zenye kuwiana na SUNNATILLAH! Tusizungumze kipuuzi juu ya nywele, ndevu, mavazi, Rasulu hakuja ili tupoteze umri kwa hukumu zinazohusu watu.
Je ni upi ufahamu wa dini unaoingilika kwa kusema kwamba hakuna mungu wala wazo la uungu pamoja na Kusudio la jina ALLAH. (La ILAHA ILLA ALLAH)?
Wanaofuja umri wao kwa kuiga bila kudadisi wala kujaribu kuelewa hili; watapigwa na bumbuwazi na kupata majuto makubwa kama matokeo ya kushindwa kuisoma hazina.
Inasikitisha kwamba ndani ya huu mfumo hakuna wazo la kufidia!.
Tahadhari: Huu ni mtazamo wangu binafsi; Haumlazimishi yeyote yule kuufuata; Apendae atachangia, asiyependa hatochangia. Kuna baadhi ya watu, kutokana na kuwa tofauti na matarajio yao wanadai kwamba tunachanganya vichwa na wanapiga marufuku tusisomwe kwa kusema kwamba “tunawafanya watu wafikirie na hivyo basi tupigwe marufuku.

Na Aisha Mbaga


UCHUMI wa MALAWI

UCHUMI-MALAWI:Kuwa ''Mwanafunzi Bora'' Kunaweza Kuwa Kubaya Kwako Pilirani Semu-Banda BLANTYRE, Aprili 17 (IPS) - Miaka mitano baada ya njaa ambapo zaidi ya watu 1,000 nchini Malawi walifariki dunia na wengine milioni 8 kati ya milioni 12 nchini humo walikabiliwa na njaa, kumbukumbu inayouma ya ushauri wa sera mbovu bado inaendelea. Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) na Benki ya Dunia zililaumiwa kutokana na janga hilo ambalo liliipiga Malawi wakati wa njaa ya mwaka 2002. Shirika la kimataifa la kupigania haki za binadamu la Action Aid, kwa mfano, lilionyesha katika taarifa ya mwezi Oktoba 2002 kwamba IMF imeitaka serikali ya Malawi kuuza akiba ya nafaka kulipia deni lililokopwa na chombo kilichosajiliwa kisheria cha Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA). Ripoti hiyo iliyojulikana kama, ‘‘State of disaster: Causes, consequences and policy lessons from Malawi'', pia ilitaja Benki ya Dunia. Action Aid iliilaumu Benki ya Dunia kutokana na ‘‘kushinikiza'' Malawi kuuza mahindi kwa Kenya kulipia deni ambalo nchi hiyo ilikuwa ikidaiwa na Benki hiyo. Halafu Waziri Bakili Muluzi pia alitangaza wazi wazi kwamba Benki hiyo imekuwa ikishawishi serikali kuhifadhi fedha za kigeni kuliko nafaka. Nafaka, Benki hiyo ilisema, zinaweza kupoteza thamani. Hata hivyo, IMF na Benki ya Dunia zilikanusha shutuma hizo kwa kusema kwamba ‘‘zilikuwa washauri tu'' kwa serikali juu ya hifadhi yake ya nafaka. Walisema kwamba sababu za uhaba wa chakula nchini Malawi zilikuwa ngumu ikiwa ni pamoja na serikali kukaa kimya kutoa onyo la haraka, kupotosha habari katika masoko ya ndani na usimamiaji mbovu wa hifadhi ya chakula. Kufuatia shutuma hizo na kujibu shutuma hizo, mahusiano kati ya mashirika ya wafadhili na serikali yaliathirika. Hii ilisababisha kuchelewa kwa wafadhili kuchukua hatua wakati wa mgogoro wa chakula. Malawi imekuwa ikitegemea zaidi wafadhili kwa miongo minne. Fedha za wafadhili ambazo imeshazipata zinakaribia asilimia 40 ya bajeti ya taifa. Nchi hiyo imeshindwa kung’ata mkono ambao unailisha. Hivyo, pamoja na madai hayo ya sababu za mgogoro wa chakula, serikali ilikamilisha mageuzi ya kiuchumi katika kuzingatia masharti yaliyowekwa na Benki hiyo na IMF. Ikiwa kama zawadi, taasisi hizo zilifutia Malawi madeni yake mengi ya nje yanayofikia dola bilioni 2.97 Septemba 2006. Kumbukumbu za njaa hiyo na sababu yake bado zinaendelea kuwepo. Baadhi ya Wamalawi wanataka nchi hiyo kujinasua kutoka kwenye mtego wa taasisi hizo. Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Jamii ya Umoja wa Mataifa, Thandika Mkandawire, ambaye yeye mwenyewe ni raia wa Malawi, ni mmoja wa watu ambao anahofia mahusiano ya nchi hiyo na nchi wafadhili na taasisi za fedha za kimataifa. Anasema pamoja na Malawi kubatizwa jina la ‘‘mwanafunzi bora'' wa Benki hiyo na IMF kati ya mwaka 1980 na 1990, nchi hiyo inasimama kama mshtaka wa mahusiano ya misaada katika miongo mitatu iliyopita. Kati ya mwaka 1979 na 1999 Malawi ilichukua nafasi miongoni mwa kile IMF ilikipatia sifa ya ‘‘mtumiaji wa muda mrefu mno'' wa vifaa vyake. Taifa hilo lilikuwa na programu sita na IMF. Miaka 17 kati ya miaka 20 Malawi ilikuwa chini ya programu moja ya IMF hadi nyingine. ‘‘Katika nyaraka za IMF na Benki ya Dunia zilizokuwa zikifanyia tathmini matokeo ya sera za uchumi wa Afrika kati ya mwaka 1981 na 1998, Malawi iko juu zaidi katika orodha ya ‘warekebishaji bora' huku ikiwa imejitokeza mara saba, ikifuatiwa na Uganda na Kenya zikiwa za tano,'' anasema Mkandawire. Pamoja na ‘‘sifa hizo'', pato la taifa la Malawi lilishuka kutoka dola za Kimarekani 156 mwaka 1980 hadi dola 143 mwaka 1990. Hata ilipofika mwaka 2003 Malawi ilikuwa bado haijafikia kiwango cha pato la taifa cha mwaka 1979, kulingana na takwimu za Benki ya Dunia. Ripoti ya umaskini na kukosekana kwa utulivu iliyotolewa mwaka jana na serikali na Benki ya Dunia inaonyesha kwamba kumekuwepo na mafanikio madogo mno katika kupunguza umaskini na kukosekana kwa usawa. Mchanganyiko wa ushauri mbovu wa kisera na utawala wa kimabavu umezalisha miongo miwili iliyopotea kwa Malawi, anasema Mkandawire. Hakupendezewa na kukubali makosa kwa taasisi hizo au Mikakati ya Benki hiyo ya Kupunguza Umaskini. Ushauri wao umesababisha kuanguka kwa uwekezaji wa umma katika mtaji wa kimaumbile na kibinadamu, anasema. ‘‘Jambo ambalo hawaonekani kulitambua ni kwamba ongezeko la makosa limesababisha uchumi ambao haujarekebishwa vizuri na kushikiliwa katika mtego wa ukuaji mdogo,'' anasema Mkandawire. Mkandawire ana wasiwasi zaidi na jinsi ya kuingiliwa na nguvu za nje kunavyosababisha mataifa ya Afrika kupoteza uhuru wake. Mwaka 2002 IMF ilisitisha misaada yake ya kiuchumi kutokana na kile ambacho imekiita usimamizi mbovu wa uchumi chini ya rais wa zamani Muluzi. IMF ilirejesha programu yake baada ya utawala wa Bingu wa Mutharika, ambaye aliingia madarakani Mei mwaka 2004, kukubali kutekeleza sera zinazosimamiwa. Kwa njia hii rikodi zinazoeleweka za kutekeleza sera ziliundwa ili kuwarejesha wafadhili. Utekelezaji wa sera kwa mwaka wa kwanza ulishuhudia IMF na Benki kuizawadia Malawi kufuta asilimia 90 ya madeni yake ya kigeni. Msamaha wa madeni ulitafsiriwa kwamba Malawi ingeokoa dola za Kimarekani milioni 100 kama akiba ya kununulia bidhaa zake kutoka nje kwa mwaka kwani nchi hiyo iliendelea kuwa na mtaji ambao ungetakiwa kutumika katika kulipia madeni. Mkuu wa sera katika Action Aid Malawi, Collins Magalasi, pia hajaridhishwa na tabia ya mashirika wahisani. Anatoa mwito kwa nchi mfadhili wakuu wa Malawi, serikali ya Uingereza, kuongeza msaada wake wa kifedha ambao katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ulifikia wastani wa pauni milioni 54.1 kwa mwaka, ambapo ni asilimia 0.0009253 tu ya pato la ndani la mwaka la Uingereza. Magalasi analaumu kuwa Wamalawi 70,000 wanafariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa yasiyozuilika. Kipato cha watu wote kikichanganywa hakilingani na ruzuku za kilimo ambayo Umoja wa Ulaya unatumia kwa wakulima wake. Wakati akielezea kuridhishwa kwake na misaada ya wafadhili ambayo nchi hiyo inapokea, Mutharika ametoa pia mwito wa ‘‘sera zinazobuniwa ndani ambazo zinapaswa kuungwa mkono na washirika wengine''. Katika mwaka wa fedha 2005/2006 serikali ilianza kutekeleza sera iliyoandaliwa ndani ya nchi iliyojulikana kama Mkakati wa Kukuza Uchumi na Maendeleo wa Malawi (MGDS), ambao utaendeshwa kwa kipindi cha miaka mitano. Mutharika anaona mkakati huo mpya kama chombo cha kuhamisha vipaumbele kwani ulibuniwa na Wamalawi. Wakati huo huo, unafanya kazi ya kurejesha nidhamu katika masuala ya fedha. Wafadhili wameunga mkono sera hiyo, kwa kukubali kuruhusu nafasi kwa sera zinazobuniwa na Wamalawi; na watu wa kawaida badala ya zile zinazobuniwa na wanauchumi na kuzimiliki. Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Haki ya Uchumi wa Malawi (Mejn), Andrew Kumbatira, anakubaliana kwamba MGDS ni sera iliyobuniwa ndani ya nchi ambapo mawazo ya ndani yamepewa nafasi kubwa mno. Anakubali kwamba ‘‘kuna sera zinazofanana na hizo katika mataifa mengine yanayoendela. Hii inaonyesha kwamba sera bado inaongozwa na wafadhili. Lakini jambo zuri kuhusu sera hii mpya ni kwamba mikutano ya ndani ya mashauriano ilikuwa mingi''. (END/2007)