Tuesday, April 10, 2007

MAGOFU YA KILWA, KIVUTIO KWA WATALII

Magofu ya Kilwa ni kivutio kwa watalii.
Na Aisha Mbaga
Magofu ya kumbukumbu ya kihistoria, ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara yanayofanyiwa ukarabati yanatarajiwa kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea eneo hilo kutoka ndani na nje ya nchi mara baada ya ukarabati kukamilika.
Mradi huo, unaendeshwa kwa pamoja na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, nchi ya Ufaransa, Japan na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utamaduni, Elimu na Sayansi (UNESCO).
Mradi huu wa maendeleo umepania kuinua utalii katika eneo hilo la lililopo kilomita 300 kusini mwa Dar es salaam.
Meneja mradi Bw.John Kimaro anasema kuwa kwa kutangaza eneo la kumbukumbu la magofu la Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kutawaelimisha wengi ambao hawajapata taarifa hizo kwa undani.
Katika ukarabati huo maeneo yanayoshughulikiwa ni pamoja na jumba la kale la Gereza “Gereza Fort” lilojengwa na Wareno mwaka 1505 na kufanyiwa ukarabati upya na Waarabu mwaka 1807,ambalo limeshawekewa umeme “security light” unaotumia nishati ya jua “solar power”.
Magofu mengine yanayofanyiwa ukarabati katika eneo hilo lenye kilomita za mraba 2000 ni Husuni Kubwa yenye eneo la mita za mraba 3000 iliyojengwa karne ya 14 na Husuni Ndogo, Jumba la Makutani “ The Makutani Palace” Msikiti Mkubwa “The Small Mosque”, Makaburi ya Shirazi “The Shirazi Tombs”, na Songo Mnara.
Mhandisi katika mradi huo Bw. Pierre Blanchard anasema kuwa ukarabati unafanywa kwa kutumia vitu asilia vilivyotumika awali katika ujenzi wa magofu hayo kama vile chokaa, udongo mwekundu, na mchanga.
Anasema kuwa iwapo ukarabati utatumia vifaa vya kisasa kama, cement, dhana nzima ya utunzaji wa magofu hayo itapotea kwa sababu haviendani na uhifadhi wake.
Ukarabati unafanywa na vijana 15 wa Kitanzania ambao wamepata mafunzo kutoka kwa watalaam wa kujitolea wa shirika lisilo la serikali la nchini Ufaransa liitwalo Chantiers, Histoire and Architecture Medievales (CHAM) linalojishughulisha na elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za kihistoria, kazi mbalimbali za kujitolea kwa vijana katika uhifadhi na mafunzo kazini kwa wale wasiokuwa na ujuzi.
Lengo la CHAM ni kuwawezesha vijana hao kupata uelewa kuhusu utunzaji wa magofu kwani baadhi yao awali walikuwa ni wavuvi au wakulima na wengine ni wasichana ambao hawajashiriki katika ujenzi kabisa.
Meneja mradi anasema kuwa kitajengwa pia kituo cha kutoa habari ili kutoa taarifa kwa wageni na watu wengine watakaokuwa na kiu ya kujua zaidi kuhusu eneo hilo la magofu lililotangazwa kuwa urithi wa Dunia mwaka 1981.
Hii ni moja kati ya hatua nyingi za kuitambulisha historia ya Kilwa kitaifa na kimataifa, na ni muhimu kwani tayari baadhi ya wadadisi wamesema kuna hatari ya vitu vilivyopo na historia yake kupotea kabisa barani Afrika iwapo havitatunzwa vizuri.
Kilwa kama ilivyo baadhi ya miji katika mwambao wa bahari ya Hindi ulikuwa ni kituo kikubwa cha biashara katika karne ya 13 na 14 hivyo kuvuta wafanyabiashara kutoka kona mbalimbali duniani.
Mji huo wa kusini ndio pekee uliokuwa na sarafu yake katika ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub Sahara Africa). Katika kipindi hicho biashara nyingi ilifanywa kwa kubadilishana vito (barter trade).
Inasemekana kuwa ingawa mambo mengi ya kale yanapatikana barani Afrika, Tanzania ikiwa moja ya nchi zenye kumbukumbu za kitamaduni za kale, wengi miongoni mwa wakazi wa Afrika hawaelewi chochote au wana uelewa kidogo mno kuhusu kumbukumbu hizo ambazo zinawahusu.
Kilwa ndiyo iliyokuwa na msikiti mkubwa katika karne ya 11 na 15 ambao hadi leo upo uliotumika wakati wa sherehe ukikusanya watu kutoka kona zote za mwambao hadi Mombasa na Sofala. Kulikuwa na misikiti 99 katika kipindi hicho ambayo baadhi magofu yake bado yapo.
Wapo wanaodai kuwa sehemu za ukanda wa kusini katika utalii zimesahaulika kabisa. Hata hivyo serikali na wahisani mbalimbali wanaboresha maeneo hayo yawe ya kuvutia zaidi kwa watalii na wageni mbalimbali mara wafikapo hapa nchini au wakiwa nje ya nchi wawe na shauku ya kufika na kujionea hazina za mambo ya kale zinazopatikana katika sehemu hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Bw. Bernad Itendele anasema kuwa wakazi wa eneo hilo wanafundishwa mambo mbalimbali ikiwamo namna ya kuwapokea watalii, kuwafunza utamaduni wao na kujifunza kutoka kwao bila woga.
Anasema kuwa wilaya hiyo imepata umaarufu katika utalii baada ya samaki aina ya Silicant zaidi ya miaka milioni 65 iliyopita kuvuliwa katika eneo hilo.
Pamoja na hayo, Mkurugenzi wa wilaya ya Kilwa, Bw. Muhando Harold Senyagwa anasema Daraja la Mkapa limeleta mabadiliko mengi, ikiwamo idadi ya wageni kuongezeka kila kukicha na upatikanaji wa usafiri wa uhakika.
Pamoja na juhudi nzuri zinazofanywa na serikali kwa kuwashirikisha wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwamo utalii wa jamii, (community tourism) ili kuinua uchumi na hali za maisha, bado juhudi kubwa zaidi inahitajika ili kufikia viwango vinavyostahili hasa katika utalii ambao kila kukicha unakua kwa kasi ya ajabu.
Baadhi ya wakala wa watalii kutoka katika nchi za ulaya wana mtizamo kuwa bado huduma ya utalii inastahili kuboreshwa ili iendane na gharama zinazotozwa, ikiwa ni pamoja na wanaojishughulisha katika kazi za utalii kuwa na elimu kuhusu shughuli zao.
Takwimu za watalii waliofika nchini kati ya mwaka 1998-2002 zinaonyesha kuwa watalii kutoka Ulaya, wengi wanatoka katika nchi za Uingereza, nchi za Scandinavia, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Holland, na Uswisi.
Inakisiwa kuwa ifikapo mwaka 2012 wageni watakaoitembelea Tanzania watafikia idadi ya watu zaidi ya 900,000 ambapo idadi hiyo kubwa ya wageni watakaofika itachangia kuongeza kipato katika sekta nyingine za uchumi.
Idadi ya wageni inaongezeka kwa sababu ya mambo mengi ikiwamo utunzaji wa vivutio vinavyopatikana hapa nchini unaofanywa na serikali na wananchi kwa ujumla hasa wale wanaozunguka maeneno ya utalii.
Aidha, Shirika la Hifadhi za Taifa la Tanzania (TANAPA) lilianzishwa mwaka 1959 pamoja na mambo mengine, kutunza hifadhi za Taifa ili zisivamiwe au kuharibiwa kwa namna yoyote kuwezesha wananchi na wageni mbalimbali kuzitembelea wakati wowote.
Kutokana na uhifadhi wa makini hasa wa maliasili Tanzania yenye eneo la kilometa za mraba 937,062 yaweza kujinadi kuwa ni moja kati ya nchi ambazo mtalii anaweza kufunga safari na kupumzika kwa kuangalia vivutio mbalimbali na kumbukumbu za zamani ambazo hazipatikani mahali pengine popote Duniani.
Katika kongamano la pili la Kimataifa la Afrika Kuhusu Nafasi ya Utalii Katika Kudumisha Amani lilofanyika hapa nchini Dr. Dawid De Villiers ambaye ni Katibu wa Shirika la Utalii la Dunia (WTO) aligusia kuwa bara la Afrika bado lina nafasi kubwa ya kufaidika na utalii, hata hivyo bado soko la sekta hiyo halijatumika ipasavyo kwa maendeleo katika jamii, bara la Afrika linawakilisha asilimia nne katika biashara ya dunia.
Alisema iko haja ya kuhakikisha picha mbaya inayolieleza bara la Afrika kama sehemu ya njaa, magonjwa na migogoro, ambapo wakati tatizo liko katika nchi moja au sehemu ndogo hali hiyo huchukuliwa iko katika bara lote.
Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri Mkuu Mhe. Frederick Sumaye alisema kuwa tukio lolote la kigaidi linapotekea ndani au nje ya Afrika huleta picha mbaya hivyo kupunguza idadi ya watalii na wawekezaji wengine hivyo kudumuza uchumi. Takwimu zinaonyesha nchi 33 kati ya 48 masikini zipo katika bara la Afrika.
Ingawa bara la Afrika lina vivutio vingi ambavyo bado havijatumika kisawasawa kwa sababu ya matatizo mbalimbali, takwimu za WTO zinaonyesha kuwa sekta ya utalii inaingiza dola za Kimarekani (USD) trillioni 3.6 na kutoa ajira moja kati ya watu 12 duniani.
Hapa nchini, na nchi nyingine za Kiafrika utalii ni moja kati ya sekta zinazotegemewa katika kuingiza fedha za kigeni hivyo kuchangia kuondoa umaskini, ambao ni mkakati wa serikali ya Tanzania kwa kuwashirikisha wananchi kuondosha umasikini.
Hata hivyo, Raisi wa Shirikisho la Sekta Binafsi la Tanzania (TPSF) Elvis Musiba aliweka bayana kuwa sekta binafsi bado “imelala usingizi” kwa sababu ya ukubwa wa mtaji unaohitajika katika kuendesha sekta hiyo.
Aliongeza kuwa matumizi mabaya ya maliasili yataleta athari kwa utalii hivyo ni muhimu kwa wananchi katika sekta binafsi kuisadia serikali katika kupambana na wahalifu waharibifu wa maliasili ili kuleta utalii endelevu
Baadhi ya tafiti kuhusu maendeleo ya Afrika zinatilia shaka bara hilo kwamba haliko sambasamba na karne ya 21 ambapo kipato katika ukanda wa Sahara (Sub Sahara Afrika) kimekuwa kidogo kuliko ilivyokuwa mwishoni mwa miaka ya 1960.
Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya Waafrika watano, mmoja yumo katika migogoro pamoja na hayo wale wenye ujuzi hukimbilia nchi za ng’ambo wakati idadi ya wakazi katika bara hilo imeongezeka mara mbili. Katika miaka 30 iliyopita.
Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa ukianza na ujenzi wa mlango wa nyasi hakika utabadilika na kumalizia kwa ujenzi wa mlango wa chuma, hivyo mradi wa ukarabati wa magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara utaleta maendeleo kwa wananchi.
mwisho

WATOTO WAPEWE MALEZI BORA WAKUWE KIAKILI

WATOTO WAPEWE MALEZI BORA WAKUWE KIAKILI
Na Aisha Mbaga
WATOTO ni mategemeo na matumaini ya wazazi na taifa lo lote linajengwa kupitia
watoto wake, lakini vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi yao ni tatizo kubwa nchini
ambalolitaendelea kupigwa vita kila kukicha.
Mtu mmoja mmoja, familia au kaya na Serikali kwa ujumla wana jukumu la kuwalinda
watoto dhidi ya ukatili na unyanyasaji.
Hii inatokana na ukweli kwamba tatizo hilo limeota mizizi, kusambaa na kujichimbia
katika jamii ambapo kwa ujumla, usalama na ustawi wa watoto hapa nchini bado ni
tatizo.
Mwishoni mwa mwaka jana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Kofi
Annan aliwasilisha katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa taarifa kuhusu utafiti juu ya
vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Tanzania ilishiriki katika utafiti huo kwa kuchangia taarifa mbalimbali katika dodoso
lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa udhamini uliofanywa na Ofisi ya Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) jijii Dar es Salaam ambayo
ilifadhili mradi wa utafiti uliofanywa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
katika wilaya 11 za Tanzania Bara.
Wilaya zilizofanyiwa utafiti huo ni Tabora, Morogoro Vijijini, Moshi Vijijini, Kilwa,
Mafia, Kibondo, Magu, Kinondoni, Lushoto, Mbinga na Mbeya.
Matokeo ya utafiti huo yalijadiliwa katika mkutano wa kitaifa wa wadau kuhusu namna
ya kuondokana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto uliofanyika
Oktoba 6 mwaka jana jijiini Dar es Salaam.
Wadau wa mkutano huo waliweka mikakati ya pamoja na kupiga vita vitendo hivyo
viovu vinavyofanywa dhidi ya watoto.
Pamoja na utafiti huo kufanyika katika wilaya 11, lakini ni ukweli usiofichika kuwa
yaliyobainika katika wilaya hizo chache, kwa kiasi kikubwa yanawakilisha taswira pana
ya tatizo hilo kwa nchi nzima.
Licha ya utafiti huo kuibua sababu nyingi za kuwepo kwa tatizo hili, hata hivyo ukweli
unaojitokeza ni kuwa hakuna sababu yo yote ile kati ya hizo inayoweza kuhalalisha
vitendo vya ukatili na unyanyasaji wanavyofanyiwa watoto.
Kwa upande Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini, Bw. Rodney Philips anaona kuwa
ripoti ya utafiti huo imehimiza Serikali ya Tanzania kuwekeza raslimali na muda wa
kutosha katika kujenga uwezo, mtandao na ushirikiano wenye lengo la kupiga vita
vitendo vya udhalilishaji watoto vitakavyojitokeza kwa namna yo yote ile.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo, Rais Jakaya Kikwete alisema, `watoto
ndio msingi wa taifa la kesho, bila ya watoto kupewa malezi na matayarisho mazuri ni
wazi kuwa taifa halina matumaini mazuri siku za baadaye...watoto nchini ni wengi mno
kiasi kwamba tusipowaangalia na kuwaandaa au kuwaandalia vizuri ushiriki wao
wawapo vijana na watu wazima taifa litakuwa limepata hasara kubwa sana.`
Kwa mujibu wa sensa iliyotolewa na Idara ya Takwimu mwaka 2004 inaonyesha kuwa
hapa Tanzania watoto ni zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wote, yaani, zaidi ya nusu ya
Watanzania ni watoto na takwimu hizi zinaonyesha kuwa kwa wastani karibu kila kaya
nchini inao watoto wasiopungua sita.
Rais Kikwete alisema ni muhimu jamii itilie maanani ukweli huu na itambue watoto ni
sehemu muhimu ya jamii, siyo kwa idadi yao tu, bali pia kwa kuwa ni binadamu
wanaostahilil kupewa haki zote za msingi.
Ili kutekeleza vita dhidi ya tatizo hilo, viongozi wa Serikali, viongozi wa kidini, taasisi
mbalimbali, asasi zisizo za kiserikali, wananchi, watoto wanatakiwa kuweka mikakati
ya pamoja kwa lengo la kukomesha au kudhibiti vitendo viovu vinavyofanywa dhidi ya
watoto.
Bw. Philips anabainisha kuwa labda unyanyasaji mkubwa dhidi ya mtoto ni ule
unaofanywa na mtu mzima mwenye kuaminiwa na kupewa heshma na mtoto, lakini
anamgeuka na kumnyanyasa na kumdhalilisha kwa kumfanyia vitendo vya ngono.
Udhalilishaji wa watoto kimapenzi ni kitendo cha kuingilia undani wa mtoto,
udhalilishaji wa kimaumbile na kisaikolojia na uvunjaji mkubwa wa maadili na kanuni
za kijamii.
Bw. Philips ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa wadau
waliokuwa wakijadili Ripoti ya Unyanyasaji wa Mtoto Oktoba mwaka jana, alisema
jamii inatakiwa kuzuia vitendo vya kuwadhalilisha watoto ambao wamekuwa
wakianguka katika dimbwi la udhalilishaji wa kimapenzi mara kwa mara.
Alisema katika mambo yote hayo, jamii inatakiwa kuliangalia suala hilo kwa umakini
zaidi hasa kwa wasichana ambao wamekuwa wakiathirika zaidi katika udhalilishaji huo.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mary Nagu anasema Tanzania itazingatia umuhimu wa
kuwa na sera madhubuti, sheria na kuwatambua watoto walio katika mazingira magumu.
Anataja umaskini, uharibifu wa mazingira na janga la Ukimwi kuwa ni maeneo
yanayohitaji nguvu ya pamoja kuyatokomeza ili watoto wawe na uhakika wa kukua na
kuishi maisha ya usalama.
Dk. Nagu anasema watoto ni zawadi kubwa kuliko zote kutoka kwa Mungu. Watoto ni
furaha ya kila aliye mzazi.
Watoto ni mategemeo na matumaini ya wazazi na taifa lo lote linajengwa kupitia watoto
wake, hivyo kuna kila ulazima wa kuwajenga na kuwalinda dhidi ya ukatili na
unyanyaswaji ili kuwahakikishia maisha yaliyo salama.
Kutokana na matokeo ya utafiti, usikilizaji hadharani, maoni na mapendekezo ya
wananchi na wadau mbalimbali kuhusu vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya
watoto, Tume ilianisha vitendo hivyo katika makundi manne ambayo ni; Unyanyasaji
kingono, Mashambulizi kimwili; Utelekezaji na Unyanyasaji wa kisaikolojia.
Katika maoni yake, Tume ilisema tatizo la unyanyasaji kingono linawaathiri zaidi
watoto wa kike kuliko wa kiume.
Utafiti huo umeonyesha kuwa sehemu kubwa ya wananchi na wadau wana uelewa wa
kutosha kuhusu aina hii ya unyanyasaji na inaonyesha ni suala linalowakera wananchi,
lakini vyombo vinavyohusika haviwajibiki ipasavyo.
Aidha baadhi ya wazazi/wananchi/walezi hawatekelezi wajibu wao ipasavyo katika
kulinda na kutetea watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kingono.
Kuhusu utelekezaji, Tume ilisema tatizo hilo limeonekana kuwa ni suala la familia
binafsi na huwaathiri watoto hao ambao ni taifa la kesho.
Imefahamika kuwa mzigo mkubwa wa kulea watoto katika familia maskini unabebwa
na kina mama. Unyanyasaji wa kisaikolojia una madhara makubwa kwa mtoto.
Hata Watoto ni mategemeo na matumaini ya wazazi na taifa lo lote linajengwa kupitia
watoto wake, lakini vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi yao ni tatizo kubwa nchini
ambalo litaendelea kupigwa vita kila kukicha.

na kina mama. Unyanyasaji wa kisaikolojia una madhara makubwa kwa mtoto. Watoto ni mategemeo na matumaini ya wazazi na taifa lo lote linajengwa kupitia watoto
wake, lakini vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi yao ni tatizo kubwa nchini ambalo
litaendelea kupigwa vita kila kukicha.

Hata akiwa mtu mzima, madhara hayo huendelea iwapo hayatapata ufumbuzi kama vile
matukio ya watoto kuchanganywa gerezani/mahabusu na watuu wazima hayamrekebishi
mtoto bali yanaongeza utukufu na usugu.
Serikali isikae kimya na kuachia hali hiyo ikiendelea, lazima ichukue hatua kali kwa
mujibu wa sheria kwa wale wote ambao wanaendeleza vitendo vya ukatili na
unyanyasaji kwa watoto.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kama chombo cha kitaifa cha kutetea,
kueneza na kulinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora nchini imekuwa
ikifuatilia kwa makini suala la haki za makundi maalumu, ikiwa ni pamoja na kundi la
watoto.
mwisho

Monday, April 9, 2007

SIGARA INAMADHARA KULIKO MOSHI WA GARI

Na aisha Mbaga
Uvutaji sigara umekuwa kama kitu cha kawaida kwa watu wengi. Watu huvuta sigara
ili kujisikia vizuri, kuchangamka, kupunguza mawazo na wengine huvuta kama
sehemu ya starehe.
Lakini, sigara au tumbaku hufanya nini miilini mwetu? Je unajua kuwa moshi wa
sigara una madhara kuliko hewa inayotoka kwenye injini za magari?
Dk. Phiilipo Kinabo wa hospitali ya Muzdalfa Yombo Vituka, anasema kuwa, wavutaji
wengi wa Sugara wamekuwa na sfya mbaya kutokana na kuathurika kwa mapafu
hivyo kusumbuliwa na ugonjwa wa TB na kusababisha vifo vingi zaidi.
Kinabo alisema kuwa, wanaoathirika zaidi ni vijana ambao wameshindwa kuacha japo
hawakuanza kuvuta kwa sababu ni dawa ama sigara inavurutubishi, lahasha , wengi
wameathirika kwa tabia za kuiga na kuhisi kuwa wanaovuta sigara ni waungwana
kuliko walevi.
pia alisema kuwa, hakuna kitu kibaya chenye kutoa moshi kinachodhuru kama moshi
wa sigara kutokana na madhara yake kuwa hasara kwa taifa. "Nashidwa kujua kwanini
Serikali inashindwa kupiga marufuku utengenezwaji wa sigara wakati inafahamu wazi
kuwa sigara inahatarisha maisha ya wanadamu wengi Diniana kote.
"Tumbaku ni jani lenye sumu aina ya nicotine ambalo hutafunwa au kuvutwa.
Tumbaku inachangamsha mwili kama ilivyo kwa sumu aina ya caffeine, ambayo
hupatikana kwenye kahawa au chai. Sumu hii, humfanya mtumiaji aizoee kwa haraka
sana. Inamchangamsha mtumiaji na kumfanya awe macho wakati mwingi. Haileweshi
lakini inapunguza hamu ya kula," alisema Dk. Kinabo
pia aliongezea kuwa Uvutaji sigara, unapunguza hewa ya oksijeni kutoka mwilini mwa
mvutaji na kusababisha mwili kutofanya kazi vizuri. Moshi wake unaharibu mishipa na
kusababisha shinikizo la damu na matatizo mengine ya moyo.
"Tumbaku ina lami, ambayo husababisha mapafu kutojisafisha vizuri na kuchangia
kupata maradhi kama vile saratani ya mapafu au koo. Huharibu ngozi na kuathiri
viumbe ambavyo havijazaliwa,"alisma Kinabo.
pia alieleza kuwa, pale mvutaji anapojikuta amekuwa mzoefu inamuwia vigumu
kuacha sigara kutokana na hali halisi, "wengi hujaribu kuacha lakini hushindwa na
kukosa raha, usingizi na kushindwa kufikiri vizuri" alisema Dk. Kinabo.
"Sumu iliyopo kwenye sigara ina madhara makubwa kwa afya. Serikali kwa kutambua
hilo, huwalazimisha watengenezaji wa sigara, kuweka onyo kali la tahadhari kwenye
paketi zao lakini hiyo haitoshi kwani bado watavuta hivyo ni vyema ikapigwa marufuku
kama ilivyo kwa bangi na mihadarati mingine," alieleza Kinabo.
"Kiungo rahisi kuathirika katika uvutaji wa sigara ni mapafu. Baada ya kuvuta moshi
wa kaboni na tindikali iliyomo kwenye tumbaku huishia kwenye mapafu ambavyo
husababisha ugumu katika kupumua na kusababisha kutunga usaha kwenye
mapafu"alisema.
"Hii huchangia kupata maambukizi mengine kama kichomi, kifua kikuu na saratani.
Nikotini vilevile ni mbaya kwa tumbo na husababisha kupoteza hamu ya kula na
maumivu katika tumbo. Watu wanaovuta mara kwa mara hutoa harufu mbaya
mdomoni na hupata matatizo ya ngozi", aliseleza Dk huyo wa mapafu.
Akilinganisha moshi wa sigara na mwingineo barabarani, twaweza kujiuliza. "Je, hewa
chafu na yenye moshi wa sigara ndani ya baa ikilinganishwa na barabarani, ambako
kuna hewa nyingi zinazotoka kwenye injini za magari, kipi kina madhara zaidi", alihoji?
Utafiti uliofanywa na wataalamu huko Marekani umedhihirisha kuwa hewa ya ndani ya
baa ina madhara zaidi. Na uchafuzi kwa hewa ya ndani ya baa au majumba ya
burudani, hautaweza kuondolewa kama watu hawatazuiwa kuvuta sigara ndani ya
majengo hayo.
Matokeo ya utafiti huo, yameonesha kuwa ikilinganishwa na ubora wa hewa iliyoko
katika barabara ambazo magari huenda kwa kasi au zile za mijini, wakati ambao kuna
msongamano wa magari, hewa iliyoko katika baa au majumba ya burudani ina
chembechembe nyingi zinazoweza kusababisha ugonjwa wa saratani kwa zaidi ya
mara hamsini.
Bw. Jeams Rapaz ni kiongozi aliyeongoza utafiti huo. Kwa mara ya kwanza aligundua
kuwa, moshi unaotoka kwenye sigara unasababisha maelfu ya watu kufariki dunia kila
mwaka.
Katika utafiti huo, Bw. Jeams Rapaz aliona kuwa, kiwango cha chembechembe
ndogo zenye uchafuzi wa mazingira katika maeneo wanakofanya kazi wafanyakazi
wa majumba ya starehe na migahawa ni cha juu sana kuliko kiwango cha uchafuzi
kinachoruhusiwa katika hewa ya nje ya majengo.
Kati ya mwezi Novemba mwaka 2002 na Januari mwaka 2003, Bw. Jean Rapaz
alifanya uchunguzi kuhusu hali ya hewa katika majumba ya starehe na migahawa sita
ya mkoani Delaware na kupima chembe za aina mbili zilizoko katika moshi wa sigara.
Matokeo yake yalionesha kuwa kuna microgram mia mbili na thelathini na moja za
chembechembe katika kila mita za ujazo, kiasi ambacho ni mara kumi na tano kuliko
kikomo cha chembe kinachoruhusiwa na mamlaka ya mazingira nchini Marekani.
Na ni mara arobaini na tisa kuliko chembe zilizoko katika barabara ya kasi ya
Wilmington, Marekani wakati wenye msongamano wa magari.
Chembe za uchafuzi za aina mbili, zenye madhara kwa afya za watu zilizoko katika
moshi wa sigara ndani ya majengo manane ya burudani wakati wa usiku zilikuwa na
microgram mia moja thelathini na nne, kiasi ambacho ni mara tano kuliko kikomo
kinachoruhusiwa katika hewa ya nje ya majengo.
Ingawa barabara ya kasi ya Wilmington, ambako kuna uchafuzi mwingi ndani ya hewa
zinazotoka kwenye injini za magari wakati wa msongamano wa magari, lakini chembe
za aina hizo ndani ya hewa ya huko ni microgram saba tu.
Kupiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, hususan katika majengo ya
burudani na migahawa ni njia nzuri. Utafiti uliofanywa umeonesha kuwa baada ya
kutolewa amri ya kupiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, chembechembe
za aina hizo zenye uchafuzi katika hewa ya majengo ya burudani yaliyotajwa hapo juu,
zimepungua kwa asilimia 90.
Utekelezaji wa sheria ya matumizi ya tumbaku na bidhaa zake nchini Marekani
adhabu dhidi ya matumizi inaanzia sh 56,250 mpaka sh milioni 1.2 au jela miezi sita
kwa wavutaji na wamiliki wa sehemu zinazovunja sheria hiyo.
Tunapaswa kujiuliza kama sheria ya udhibiti wa bidhaa za tumbaku iliyopitishwa
bungeni hapa nchini inatiliwa maanani. Kifungu cha kumi na mbili cha sheria hiyo
kinazuia uvutaji ua utumiaji wa bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma bali
vitendo hivyo bado vinashuhudiwa.
Utalii Ukiwezeshwa Tutaendelea
Na Aisha Mbaga
SERIKALI inaposhauriwa katika mabo yanayoendeleza nchi, nivyema ikatilia mkazo kwani wakati mwingine huwa ushauri unafaida kwa taifa,
kama tunakumbuka kipindi cha uongozi wa serikali ya Dk Salmin Amou, alitoa uamuzi wa kuruhusu sekta ya utalii Visiwani iendelezwe lakini mwanzoni uamuzi huo ukipingwa na wengi ikiwa ni pamoja na kulalamikiwa na baadhi ya wananchi ambao hawakuwa wakielewa vyema matokeo yake.
Kwa sasa wananchi wengi wanaona faida ya uamuzi huo na wengi wameuunga mkono kutokana na sekta hiyo kuleta matunda kwa wananchi wa Zanzibar na serikali kwa ujumla .
Rais Mstaafu Dk Salmin Amour na serikali yake walifikia uamuzi wa kuruhusu sekta ya utalii kuchipua mwaka 1992 kama njia ya kuongeza vyanzo vya mapato na kuinua hali za maisha ya wananchi wake.
Kutokana na umuhimu wa sekta hiyo, mwaka 1996, Dk Salmin aliamua kuanzisha kamisheni ya Utalii na kutunga sheria No. 9 ya mwaka 1996 ambayo inasimamia sekta hiyo.
Uamuzi huo, uliwashtua watu wengi na kupata upinzani wa chini kwa chini kwa vile faida zake zilikuwa hazionekani wakati huo.
Hatua hiyo, ilisababishwa na wasiwasi wa baadhi ya wananchi kuwa suala hilo linahusu mila na utamaduni, na kuhofia kuathirika kwa utamaduni wa Mzanzibari.
Hata hivyo malengo ya Dk. Salmin yalionekana tofauti na mawazo yao, kwa vile sekta hiyo hivi sasa imeleta faida kubwa kwa serikali na wananchi wake baada ya bei ya zao la karafuu kuporomoka katika soko la dunia.
Zao la karafuu lilitegemewa sana katika kuchangia pato la taifa tangu utawala wa kifalme wa Sultani na baada ya mapinduzi ya Zanzibar kwa vile mzunguko mkubwa wa fedha kwa wananchi wake ulitegemea zao hilo.
Mwenyeketi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZTC) Issa Ahmed Othman anasema sekta ya utalii Zanzibar kwa sasa inachangia asilimia 20 ya pato la taifa kutokana na watalii wanaotembelea Zanzibar kutoka nchi mbalimbali duniani hasa Ulaya.
Anasema kuwa kuanzia mwezi wa Julai hadi Desemba mwaka jana, watalii wapatao 135,000 walitembelea Zanzibar, kiwango ambacho ni kikubwa kulinganishwa na watalii 125,443 waliotembea Zanzibar kipindi kama hicho mwaka 2005.
Alisema katika kipindi cha Januari pekee mwaka huu, watalii 14,117 walitembelea Zanzibar, kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika kipindi cha mwezi mmoja kutembelewa na idadi kubwa ya watalii kama hiyo.
Mwenyekiti alisema kuwa, zipo sababu tatu za kuimarika sekta ya utalii Zanzibar, ikiwemo kwamba Zanzibar haina majanga ya kutisha, utulivu wa kisiasa, pamoja na kuwa na maeneo mengi yanayowavutia watalii.
Hata hivyo alisema, sekta hiyo inakabiliwa na matatizo makubwa mawili, kukosekana kwa watu wenye taaluma ya juu katika sekta ya utalii, kukosekana kwa soko la vyakula na matunda na hivyo kulazimika kutegemea kutoka nje ya Zanzibar.
``Sekta ya utalii ina tatizo la ukosefu wa watu wenye taaluma ya utalii na kulazimika nafasi nyingi kushikwa na watu kutoka nje ya Zanzibar,`` Akasema Mwenyekiti huyo.
Alisema kuwa, wakati Chuo cha Utalii Zanzibar- Maruhubi, kinatoa wanafunzi wenye kiwango cha cheti, uwekezaji wa utalii Zanzibar unakua na unahitaji watu wenye taaluma ya stashahada na shahada ya Chuo Kikuu.
Aidha alisema kwamba kumefika wakati Zanzibar iwe na shirika lake la ndege, kwa vile ina uwezo wa kulitumia soko hilo kwa watali wanao safari kati ya Zanzibar na mataifa ya Ulaya na Tanzania Bara.
``Watalii wanaosafiri kati ya Zanzibar na mikoa ya Tanzania Bara kuangalia vivutio vya utalii, bado hawana uhakika wa usafiri wa anga kwa vile ndege zinazotumika ni ndogo,`` Anasema Mwenyekiti.
Alisema kuwa, ni kweli Zanzibar ina mchango wake katika Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) lakini tangu shirika hilo kubinafsishwa, na Serikali ya Muungano, limeimarisha zaidi safari zake kati ya Tanzania na Afrika Kusini wakati watalii wanatembelea Zanzibar wanatoka nchi za Magharibi na Ulaya.
Alisema kwamba, pamoja na mafanikio yaliyopatikana, sekta ya utalii Zanzibar inahitaji kuimarishwa katika sekta ya ulinzi ili kuwaondolea usumbufu watalii.
``Utaratibu wa kuwafanyia upekuzi watalii kwa kufungua mabegi yao na kuyapekua, umepitwa na wakati, lazima tuwe na vifaa vya kisasa ili tusiwapotezee muda wao wanapopita uwanja wa ndege,`` alisema Bw Othman.
Hata hivyo alisema ni kweli unapowakawiza wawekezaji, kuna faida na hasara lakini la msingi ni kuendelea kuheshimu mila na utamaduni.
``Unapokaribisha uwekezaji, ni sawa na kufungua dirisha, kila mdudu ataingia wakiwemo mbu na inzi. Cha msingi ni kuheshimu mila na utamaduni kama kweli tunataka kuwa na jamii bora `` Anasema Mwenyekiti huyo.
Akasema kwamba jambo la msingi lazima wanaume wakubali kubadili tabia, kwa vile wao ndio wanaoimarisha biashara ya ukahaba, na sio haki kuwachukulia hatua wanawake wanaojiuza kwa kutumia vibaya sekta ya utalii.
Aidha anasema kwamba, sekta ya utalii hadi hivi sasa inahitaji kuwa na mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kutoka katika sekta hiyo ili takwimu sahihi ziwe zinapatikana.
Akasema kuwa hivi sasa vyombo ni vingi vinavyokusanya mapato, ikiwemo Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Baraza la Manispaa, Halmashauri za Wilaya, pamoja na jumuiya zisizokuwa za serikali zinazojishughulisha na sekta hiyo.
Anasema kwamba, sera ya utalii iliyopitishwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, itafanikiwa kama taasisi zote za serikali zitaamuwa kuimarisha sekta za miundo mbinu, kilimo na uvuvi, ili Zanzibar iondoke katika kutegemea bidhaa za vyakula kutoka Tanzania bara katika soko hilo.
Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Bw Mohamed Ismail anasema kwamba wameamua kufanya ukaguzi usiku katika mahoteli ya kitalii baada ya kujitokeza vitendo vya udangayifu kwa wawekezaji.
Akasema kwamba maafisa wa bodi hiyo, wamekuwa wakifanya kazi saa 24, ikiwemo kukagua vyumba vya hoteli ambavyo havina wageni ili kuweka kumbukumbu sahihi za ulipaji kodi.
``Kuna baadhi ya wafanyabiashara, walikuwa wanapokea wageni 200 kwa siku, lakini wanalipia kiwango kidogo cha wageni, na utaratibu huu wa kufanya ukaguzi umetusaidia sana,`` Akasema kamishna Ismail.
Akasema kwamba, ukusanyaji wa mapato Zanzibar umeongezeka kwa asilimia 105.4 kutoka mwaka 1999 hadi mwaka wa fedha wa 2005/2006.
Akasema katika mwaka huu wa fedha bodi hiyo inatarajia kukusanya sh bilioni 60 kutoka sh bilioni 44.3 ambapo kila mwezi wanatarajiwa kukusanya sh bilioni tano badala ya sh bilioni 3.5.
Alisema kwamba, fedha hizo zinatoka katika vyanzo vitatu vya mapato ikiwemo sekta ya Utalii,mafuta na biashara.
Hata hivyo, baadhi ya wananchiZanzibar,wanasema sekta ya utalii Zanzibar imeyumbisha mila na utamaduni wa Mzanzibari kwa vile mavazi mengi wanaovaa vijana wakiwemo wasichana hayana tofauti na wanayovaa watalii wanayotoka nchi za ulaya.
``Zanzibar haikuwa rahisi kumuona msichana kavaa nguo fupi kitovu wazi,au nywele wazi, lakini hivi sasa ni vitu vya kawaida , na tunaamini hali hii imechangiwa na utandawazi katika sekta ya utalii,``Akasema Bw Abdulrahman Saleh mkazi wa Mkunazini.
Sheikh Suleiman Masoud wa Mtaa wa Kiponda anasema kuwa pamoja na sekta ya utalii kutoa mchango mkubwa, bado serikali inapasa kuwaeleimisha watalii wanapofika Zanzibar kuvaa nguo za heshima wanapotembelea mitaa mbalimbali hasa mji mkongwe.
``Tunaifundisha jamii yetu nini, kama wageni wanapita mitaani huku nguo za ndani zikionekana?
Tusijaribu kuacha utamaduni wetu, bado muda wa kuwaelimisha wageni upo,`` Akasema Zainab Kombo mkazi wa Vuga.
Pamoja na kuimarika kwa sekta ya Utalii Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ),bado inahitajika kuimarisha Chuo cha Utalii kilichopo Marhubi, ili vijana waweze kunufaika na sekta badala ya kuajiri vijana kutoka nchi jirani za Kenya, na Uganda.
Aidha sheria ya kazi No 3 ya mwaka 1997,na marekebisho yake lazima isimamiwe vizuri na kamisheni ya kazi Zanzibar ili iweze kuwanufaisha wafanyakazi wazalendo, ambao wana tofauti za mishahara kwa asilimia zaidi ya 80 na wafanyakazi wenzao wageni.
Pamoja na sheria hiyo, kuwapa uwezo maafisa wa kamisheni ya kazi kuhakikisha mikataba ya kazi wanaikagua kabla ya kufikiwa, kati ya wawekezaji na wafanyakazi wa kizalendo,lakini mikataba isiyozingatia sheria imeendelea kuwa kero katika sekta hiyo.
Wafanyakazi wengi wa kizalendo, wamekuwa wakifungishwa mikataba ya muda mfupi na kushindwa kunufaika na sheria ya mfuko wa Hifadhi wa Jamii Zanzibar,(ZSSF),kutopatiwa posho ya likizo, nyumba, matibabu, pamoja na malipo ya kazi za ziada.
mwisho