Monday, April 9, 2007

SIGARA INAMADHARA KULIKO MOSHI WA GARI

Na aisha Mbaga
Uvutaji sigara umekuwa kama kitu cha kawaida kwa watu wengi. Watu huvuta sigara
ili kujisikia vizuri, kuchangamka, kupunguza mawazo na wengine huvuta kama
sehemu ya starehe.
Lakini, sigara au tumbaku hufanya nini miilini mwetu? Je unajua kuwa moshi wa
sigara una madhara kuliko hewa inayotoka kwenye injini za magari?
Dk. Phiilipo Kinabo wa hospitali ya Muzdalfa Yombo Vituka, anasema kuwa, wavutaji
wengi wa Sugara wamekuwa na sfya mbaya kutokana na kuathurika kwa mapafu
hivyo kusumbuliwa na ugonjwa wa TB na kusababisha vifo vingi zaidi.
Kinabo alisema kuwa, wanaoathirika zaidi ni vijana ambao wameshindwa kuacha japo
hawakuanza kuvuta kwa sababu ni dawa ama sigara inavurutubishi, lahasha , wengi
wameathirika kwa tabia za kuiga na kuhisi kuwa wanaovuta sigara ni waungwana
kuliko walevi.
pia alisema kuwa, hakuna kitu kibaya chenye kutoa moshi kinachodhuru kama moshi
wa sigara kutokana na madhara yake kuwa hasara kwa taifa. "Nashidwa kujua kwanini
Serikali inashindwa kupiga marufuku utengenezwaji wa sigara wakati inafahamu wazi
kuwa sigara inahatarisha maisha ya wanadamu wengi Diniana kote.
"Tumbaku ni jani lenye sumu aina ya nicotine ambalo hutafunwa au kuvutwa.
Tumbaku inachangamsha mwili kama ilivyo kwa sumu aina ya caffeine, ambayo
hupatikana kwenye kahawa au chai. Sumu hii, humfanya mtumiaji aizoee kwa haraka
sana. Inamchangamsha mtumiaji na kumfanya awe macho wakati mwingi. Haileweshi
lakini inapunguza hamu ya kula," alisema Dk. Kinabo
pia aliongezea kuwa Uvutaji sigara, unapunguza hewa ya oksijeni kutoka mwilini mwa
mvutaji na kusababisha mwili kutofanya kazi vizuri. Moshi wake unaharibu mishipa na
kusababisha shinikizo la damu na matatizo mengine ya moyo.
"Tumbaku ina lami, ambayo husababisha mapafu kutojisafisha vizuri na kuchangia
kupata maradhi kama vile saratani ya mapafu au koo. Huharibu ngozi na kuathiri
viumbe ambavyo havijazaliwa,"alisma Kinabo.
pia alieleza kuwa, pale mvutaji anapojikuta amekuwa mzoefu inamuwia vigumu
kuacha sigara kutokana na hali halisi, "wengi hujaribu kuacha lakini hushindwa na
kukosa raha, usingizi na kushindwa kufikiri vizuri" alisema Dk. Kinabo.
"Sumu iliyopo kwenye sigara ina madhara makubwa kwa afya. Serikali kwa kutambua
hilo, huwalazimisha watengenezaji wa sigara, kuweka onyo kali la tahadhari kwenye
paketi zao lakini hiyo haitoshi kwani bado watavuta hivyo ni vyema ikapigwa marufuku
kama ilivyo kwa bangi na mihadarati mingine," alieleza Kinabo.
"Kiungo rahisi kuathirika katika uvutaji wa sigara ni mapafu. Baada ya kuvuta moshi
wa kaboni na tindikali iliyomo kwenye tumbaku huishia kwenye mapafu ambavyo
husababisha ugumu katika kupumua na kusababisha kutunga usaha kwenye
mapafu"alisema.
"Hii huchangia kupata maambukizi mengine kama kichomi, kifua kikuu na saratani.
Nikotini vilevile ni mbaya kwa tumbo na husababisha kupoteza hamu ya kula na
maumivu katika tumbo. Watu wanaovuta mara kwa mara hutoa harufu mbaya
mdomoni na hupata matatizo ya ngozi", aliseleza Dk huyo wa mapafu.
Akilinganisha moshi wa sigara na mwingineo barabarani, twaweza kujiuliza. "Je, hewa
chafu na yenye moshi wa sigara ndani ya baa ikilinganishwa na barabarani, ambako
kuna hewa nyingi zinazotoka kwenye injini za magari, kipi kina madhara zaidi", alihoji?
Utafiti uliofanywa na wataalamu huko Marekani umedhihirisha kuwa hewa ya ndani ya
baa ina madhara zaidi. Na uchafuzi kwa hewa ya ndani ya baa au majumba ya
burudani, hautaweza kuondolewa kama watu hawatazuiwa kuvuta sigara ndani ya
majengo hayo.
Matokeo ya utafiti huo, yameonesha kuwa ikilinganishwa na ubora wa hewa iliyoko
katika barabara ambazo magari huenda kwa kasi au zile za mijini, wakati ambao kuna
msongamano wa magari, hewa iliyoko katika baa au majumba ya burudani ina
chembechembe nyingi zinazoweza kusababisha ugonjwa wa saratani kwa zaidi ya
mara hamsini.
Bw. Jeams Rapaz ni kiongozi aliyeongoza utafiti huo. Kwa mara ya kwanza aligundua
kuwa, moshi unaotoka kwenye sigara unasababisha maelfu ya watu kufariki dunia kila
mwaka.
Katika utafiti huo, Bw. Jeams Rapaz aliona kuwa, kiwango cha chembechembe
ndogo zenye uchafuzi wa mazingira katika maeneo wanakofanya kazi wafanyakazi
wa majumba ya starehe na migahawa ni cha juu sana kuliko kiwango cha uchafuzi
kinachoruhusiwa katika hewa ya nje ya majengo.
Kati ya mwezi Novemba mwaka 2002 na Januari mwaka 2003, Bw. Jean Rapaz
alifanya uchunguzi kuhusu hali ya hewa katika majumba ya starehe na migahawa sita
ya mkoani Delaware na kupima chembe za aina mbili zilizoko katika moshi wa sigara.
Matokeo yake yalionesha kuwa kuna microgram mia mbili na thelathini na moja za
chembechembe katika kila mita za ujazo, kiasi ambacho ni mara kumi na tano kuliko
kikomo cha chembe kinachoruhusiwa na mamlaka ya mazingira nchini Marekani.
Na ni mara arobaini na tisa kuliko chembe zilizoko katika barabara ya kasi ya
Wilmington, Marekani wakati wenye msongamano wa magari.
Chembe za uchafuzi za aina mbili, zenye madhara kwa afya za watu zilizoko katika
moshi wa sigara ndani ya majengo manane ya burudani wakati wa usiku zilikuwa na
microgram mia moja thelathini na nne, kiasi ambacho ni mara tano kuliko kikomo
kinachoruhusiwa katika hewa ya nje ya majengo.
Ingawa barabara ya kasi ya Wilmington, ambako kuna uchafuzi mwingi ndani ya hewa
zinazotoka kwenye injini za magari wakati wa msongamano wa magari, lakini chembe
za aina hizo ndani ya hewa ya huko ni microgram saba tu.
Kupiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, hususan katika majengo ya
burudani na migahawa ni njia nzuri. Utafiti uliofanywa umeonesha kuwa baada ya
kutolewa amri ya kupiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, chembechembe
za aina hizo zenye uchafuzi katika hewa ya majengo ya burudani yaliyotajwa hapo juu,
zimepungua kwa asilimia 90.
Utekelezaji wa sheria ya matumizi ya tumbaku na bidhaa zake nchini Marekani
adhabu dhidi ya matumizi inaanzia sh 56,250 mpaka sh milioni 1.2 au jela miezi sita
kwa wavutaji na wamiliki wa sehemu zinazovunja sheria hiyo.
Tunapaswa kujiuliza kama sheria ya udhibiti wa bidhaa za tumbaku iliyopitishwa
bungeni hapa nchini inatiliwa maanani. Kifungu cha kumi na mbili cha sheria hiyo
kinazuia uvutaji ua utumiaji wa bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma bali
vitendo hivyo bado vinashuhudiwa.

No comments: