Tuesday, May 22, 2007

Na Aisha Mbaga
Mambo vipi msomaji wangu wa safu ya Mahaba? Natumai kwa uwezo wa Mwenyezii Mungu umzima wa afya na waendelea vyema katika maandalizi ya mwanzo wa wiki.
natumai wiki iliyopita tuliangalia jinsi ya maandalizi ya wakati wa tendo la kujamiaana.
ninaimani nimeeleweka kwa wale waelewa. nawashukuru walionipigia simu kunipongeza na kunitaka ushauri.
Dada yangu salha wa Arusha ananiuliza jinsi ya kumlea Mwanaume, usijali, Salha kwani mwanaume mbele ya mwanamke ni sawa na mtoto mdopgo, waweza mliza upendavyo ila unachotakiwa ni kuwa mbunifu.
Leo tutazingumzia mambo muhimu katika kufikisha hisia zako. wapo baadhi ya watu hawawezi kumweleza mwanaume ukweli kuwa anampenda na matokeo anabaki akiumia bila kujua la kufanya. kwa upende wangu mimi sioni aibu endapo najikuta nipo penzini nakiwa mwazi.
jambo la kufanya kwa mwanaume umpendaye naye hajui kuwa unampenda, kwanza mwambie kama uwezo wa kufanya hivyo unao. wapo wanawake jasiri kwa kuweka mambo bayana na kujikuta wengine wanafanikiwa kutatua matatizo yao. baadhi ya watu wanaamini kuwa, kumweleza mwanaume ukweli kuwa unampenda ni utamaduni wa wazungu, mimi naamini kuwa katika hisia hakuna mzungu wala mwafrika.
Endpo huwezi kuweka mambo bayana tumia nwiki wako kuhakikisha kuwa unamteka mwanaume huyo kwa kumtega kwa kutumia njia tano muhimu
njia ya kwanza kuweza kumtega mwanaume ni mavazi.
unaweza kumtega mwanaume unayempenda kw akuimia mavazi, jaribu kuvaa vivazi vya kumvutia na kumfanya atahamaki kwa kukuwaza kila amapo kumbuka kivazi chako.
fanua jitikada za kujipitisha pitisha kila mara kwake huku ukiwa na vizawadi ambavyo vitamfanya awe rafuki yako na kumweleza wazi kuwa unapenda kuwa karibu naye hatakama hataki kuwa mpenzi wako.
jia ya pili, pendelea kutoka naye kila wakati ikiwa ni moja ya njia ya kumhamasisha na utokapo kuwa unamshangaza kwa kumpa zawadi ama kumwandalia chakila maakum ambacho unauhakika atakipenda na kitamvutia.
tumia sauti yako katika mazungumzo ili aweze kuvutika nayo kwani katika mahusiano, sauti inaweza kuchukua nafasi kumshawishi mwanaume na kujikuta akiiwaza na kuingia mtegoni.
pia hakikisha kuwa macho yako yanazungumza kwa kumtazama na kila ayaonapo ataona vimrlea vya mapenzi ndani ya mboni ya jicho lako na kujikuta kuwa anasogea karibu na wakati mwingine anaweza kukushangaza kwa kukuambia kuwa anakupenda japo hakuwa tayari kuwa na wewe.
wakati mwingine si lazima mwanaume aanza kupenda hata wanawake wanapenda na wananafasi ya kuonyesha mapenzi yao na kuhangaika hadi kufanikisha penzi lake kw ayule ampendae.
kwa leo tuishie hapo na usikose kuungana nami wiki ijayo. Alamsiki
kwa maoni na ushauri wasiliana nami kwa simu 0755690690, ama barua pepe yangu aishamudysaan@yahoo.com pia unaweza kupitia website yangu, mudysaa.blogspot.com

No comments: