Tuesday, May 22, 2007

Aisha Mbaga

MbagaMambo vupi mpenzi msomaji wa safu hii ya mahaba? natumai kwa uwezo wa Mungu amekujaalia pumzi na umzima wa afya hapo ulipo unaungana nami katika mambo ya mahaba.
kama ilivyo ada ya mapenzi kuwa ni makubaliano kati ya wawili basihakuna haja ya kulazimishana katika kufanya mapenzi, hii ndiyo mada yetu ya leo.
Ukipendana na mtu kwa dhati, mtaheshimiana, hutafanya kitu chochote cha kumwuudhi au kumwuumiza, hutamlazimisha mwenzio kufanya kitu ambacho hapendi au hataki na wakati wote utataka kumfurahisha.
Kitu kimojawapo ambacho kitakutokea wakati unakua ni kuwa na mpenzi aliyekuingia moyoni au kupata mapenzi mazito.
Kumpenda mtu kunaweza kuwa kuzuri. Lakini mara nyingine kunaweza kukuchanganya akili hususan yanapojitokeza mambo ya kufanya mapenzi.
Wapo ambao wanafurahia mapenzi kwa kuwa wanapendana na wenzi wao lakini pia wapo wanaotamani kufa ama kujuta kuzaliwa kwa kuwana wapenzi ambao hawajatulia.
Ili kuepukana na majonzi hakikisha kuwa unayempenda naye anakupenda kisha hana papara ya ngono.
lama kwli anakupenda atakuvumilia nawe hakikisha kuwa unakuwa na msimamo wa kutofanya ngono hadi uwe tayari. ZIngatia mambo yafuatayo ikimpata mpenzi ili kuhakikisha kuwa unamsoma na kuupa moyo wako nafasi ya kufanya maamuzi.
LAZIMA MFANYE NGONOUkiwa na mpenzi unayempenda kwa dhati haina maana kwamba ni lazima mfanye nae mapenzi. Kitendo cha kufanya mapenzi kinatakiwa kiheshimiwe na kipewe hadhi yake kwa hivyo usikiendee kwa papara!
SUBIRI mpaka ukiwa tayari kimaumbile na kimawazo. Unaweza kuanza kufanya mapenzi ukiwa katika mapenzi ya dhati na ambayo unayaona yanaweza kumudu vishindo vyote.
USIKUBALI KUDANGANYWAUkiangalia filamu karibu zote zinazooneshwa siku hizi au ukizungumza na marafiki zako unafikiria kwamba kila mtu anafanya mapenzi wakati wote. Hii sio kweli kabisa! Watu wengi wanasubiri mpaka watakapokuwa watu wazima au wakishaolewa au kuoa.
EPUKA UONGO KATIKA MAPENZIUwapo utaweza kuwa mkweli kwa huyo unayemtarajia, ni wazi kuwa mnaweza kuelewana na ni rahisi sana kugundua tabua zake kwa kuwa wakati wote utakuwa mwazi kwake naye atajutahidu kuwa wazi na ukiona mpenzi wako ni mwongo basi hakufai tafuta njia ya kumfanya awe mkweli ama heri kukaa na kumtafuta mkweli kwani baadae unaweza kujutia mahusiano yako.
Unaweza kumpenda mpenzi wako na kuamua kutofanya naye mapenzi. Kama mpenzi wako anakupenda kwa dhati basi ataheshimu uamuzi wako na atakuwa mkweli kwako ikiwa ni pamoja na kukutunzia heshma yako.
pamoja na mila na desturi za Waafrika, mwanamke ameonekana kwa yeye ndiye anayelazimishwa kufanya ngono wakati hawako tayari, Hata wavulana wanalazimishwa kufanya mapenzi na wapenzi wao au hata marafiki zao. Sio vizuri kwa marafiki kuwashawishi wasichana au wavulana kufanya mapenzi wakati wao hawako tayari.
basi kwa leo tuoshie hapa ila usisahau kujiunga nami wiki ijayo,kwa waswaki na maoni wasiliana namoi kwa barua pepe yangu aishamudysaan@yahoo.com.

No comments: