Friday, March 16, 2007

mapenzi ni nguzo ya kujenga familia

Na Aisha Mbaga

Mengi yameongelewa na yatazidi kuongelewa kuhusiana na hali halisi katika uwanja wa mapenzi.

Mimi nazungumzia hali hiyo lakini katika upande wa kuanzisha , kuboresha na kuyalinda mapenzi ya dhati.

Nimekusudia kukutandikia uwamja huu kwa sababu mapenzi ni kitu kisichokwepeka.

Hakuna binadamu anayeweza kukyakwepa mapenzi, kukwepa kupenda ama kupendwa kutokana na kuwa hayo ni maumbile.

Kwa kawaida mtu umpendae kuwa hukosi hamu ya kuonana naye kama ilivyo kwa mama na mwana ama mwana na mama ila katika mapenzi ya msichana na mvulana mambo hubadilika na kuwa ya ndani zaid.

Ukiwa na hamu ha hali ya juu kwa mpenzio basi upo katika kilele cha mapenzi na hutakiwi kushuka kwani ukiona unashuka kiwango cha kumuona mpenzio basi ujue kunahatari ya kusambaratika kwa mapenzu yenu.

Napenda kuanzia kukiandaa chumba cha mapenzi, ama uwanja wa mapenzi. Si lazima iwe kitandani tu, waweza badili uwanja kwa kuhamia bafuni ama kochini nap engine gaeini.

Kwanza kisafishe chumba chako vizuri kwa kifita vumbi kila kona .

Hakikisha kuwa unakipamba chumba chako kwa mauwa na kadi kama unazo.

Kifukize chumba chako udi ili kukifanya kinykie vizuri ama kipulizie marashi ya sluud kama unauwezo nayo, kama huna waweza tumia hata air freshna.

Kinachotakiwa ni kuiandaa sehemu yenyewe. Kama kitandani, tandika kitanda chako vizuri kwa shuka lemuye mauwa ya kuvutia, kama ni jeupe na halina mauwa, waweza kuchukua mauwa ya asumini ukayamwaga kitandani bna kuyatandaza vizuri. Ukikosa asumini waweza tumia mauwa ridi,. Mauwa haya huwa yanaharufu nzuri.

Waweza yatandaza nyumba nzima kama waweza ama chumba kizima kiwe kinanukia asumini,

Baada ya hapo hakikisha kuwa unausafisha mwili wako vizuri na kuuweka safi kwa ajili ya kuingia uwanjani kucheza mechi ya mahaba.

Fahamu kuwa kunamaks ambazo unaweza kuzipata ukiwa uwanjani ama ukazikosa hivyo ili kujiweka katika kiwango cha juu cha ufundi wa kufunga magoli ya mapenzi, ni lazima uwe na juhudi, usichoke na uwe makini katika mchezo ili uhakikishe mnatoka sare kwa kufunga goli.

Kwa kufanya hivyo utakuwa umefaulu mechi yako na utajiweka katika nafasi ya juu kiasi cha kumfanya mpenzio kukukumbuka kila awapo.

Sasa nakupeleka katika kuuandaa mwili wako.

Nenda bafuni uoge vizuri na ujisafishe sehemu zako zote nyeti za mili vizuri kwa kuuweka mili wako safi ili mpenzio aweze kuutembelea apendavyo.

Jitie manukato laini. Jifukize ikili yako udi na hakikisha kuwa wakati wa kujifukiza unamimina marashi ya aluud ili kuiruhusu harufu nzuri kupenya sehemu zote.

Fukiza nyele zako na nguo zako utakazovaa kabla ya kuingia uwanjani.

Andaa kitezo chako na moto kisha kiweke udi na uendelee kupendezesha chumba chako.

Andaa kitambaa cha pamba, mji ya mojo kwenye chupa na kibeseni kwa ajili ya kujisafisha mara baada ya mechi wewe na mpenzio.

Aingiapo mpenzio tia marashi ya aluud kwenye kitezo kisha mkaribishe uwanjani na muanze na mazoezi kabla ya mechi kali.

Wakati mnaendelea na mechi udi na marashi ya aluud yanapenya kwenye miili yenu taratibu na kuburudisha.

Kumbuka kutumia kitambaa chako laini kujisafishia taka zote baada ya mechi kali kisha nendeni wote bafuni mkaoge. Ikiwezekana endeleeni kujipa raha humohumo bafuni.

Ka leo tuishie hapo ila nakusihi usikose kujiunga nami toleo lijalo. Kwa maoni ushauri, wasiliana nami kwa barua pepe. aishamudysaan@yahoo.com au simu ya kiganjani 0755690690.

No comments: